Tuesday, September 18, 2012

KUTOKA WIZARA YA ELIMU: WARAKA WA ELIMU NA.5 WA MWAKA 2012 KUHUSU MAREKEBISHO YA MIHULA YA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU


Tangu mwaka 2005 kumekuwepo na tatizo la kutofautiana kwa Mihula ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mpaka cha Nne, Kidato cha Tano na Sita na Vyuo vya Ualimu. Aidha, kipindi cha kufanya mitihani ya Taifa katika kidato cha Nne na Sita hutofautina. Vilevile, usahihishaji wa mitihani ya ngazi hizo za elimu umekuwa ukifanyika wakati baadhi ya makundi ya wanafunzi wakiendelea na masomo Shuleni/Vyuoni.

Usahihishaji wa mitihani wakati baadhi ya makundi ya wanafunzi wakiendelea na masomo umekuwa ukiathiri maendeleo ya wanafunzi kimasomo. Wasahihishaji wa mitihani hiyo wamekuwa na muda mrefu wa kufanya kazi hiyo na kukosa muda wa kupumzika na kujikuta wanafanya kazi hiyo kwa mfululizo mwaka mzima. Hali hiyo imesababisha baadhi ya walimu kushindwa kufanya kazi za kitaaluma ipasavyo.

Ili kurekebisha hali hiyo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeamua kurekebisha Mihula ya shule; ili wanafunzi wa ngazi zote katika shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu wawe na vipindi vya likizo vinavyofanana.

Aidha, urekebishaji wa Mihula utaendana sambamba na marekebisho ya vipindi vya mitihani ya Taifa katika ngazi hizo kama ifuatavyo:
Tanbihi: Wanafunzi wote watapumzika Mwezi Juni na Desemba. Waraka huu, unaanza kutumika tarehe 01 Januari, 2013 na kufuta Waraka wa Elimu Na. 5 wa Mwaka 2004
 
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
Katibu Mkuu,
OWM -TAMISEMI,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
Mkurugenzi,
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima,
S.L.P. 20679,
DAR ES SALAAM.
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Elimu Tanzania
S.L.P. 35094,
DAR ES SALAAM.
Katibu Mtendaji,
Baraza la Mitihani la Tanzania,
S.L.P. 2624,
DAR ES SALAAM.

VIBE QUOTE OF THE DAY: HAPPINESS IS ONLY REAL, WHEN SHARED


FEDHA ZA MIKOPO BADO KITENDAWILI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NCHINI, WAKATI VYUO VIPO MBIONI KUFUNGULIWA


Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, wako hatarini kuchelewa kupata fedha za mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutokana na mchakato wa kutoa mikopo hiyo kuchelewa kuanza.

Hali hiyo inatokana na vyuo hivyo kuanza kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao.  Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE umebaini kuwa wanafunzi katika vyuo hivyo walioomba mikopo toka HESLB, bado hawajaanza kupata hatua ambayo imeanza kuwapa shaka kama wataripoti vyuoni kwa wakati kutokana na kutegemea fedha za mikopo kwa ajili ya ada ya masomo na mahitaji mengine.

Kutokana na ucheleweshaji wa mikopo hiyo, gazeti hili lilishudia wanafunzi kadhaa ambao wamedahiliwa kujiunga vyuo vya elimu ya juu mwaka huu, wakimiminika katika ofisi za HESLB makao makuu jijini Dar es Salaam kuulizia hatma ya mikopo waliyoomba.

“Unavyoniona hapa ni wiki ya tatu nimekuwa nikija hapa ofisi za Bodi ya Mikopo kuulizia kama mikopo imeanza kutolewa, lakini tunaelezwa tuendelee kusubiri wakati vyuo vimekaribia kufunguliwa,” alisema mwanafunzi mmoja aliyetoka Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

Hata hivyo, Afisa mmoja wa HESLB, aliyejitambulisha kwa jina moja la Venelanda, alisema mchakato wa kuandaa mikopo ya wanafunzi bado unaendelea na kwamba zoezi hilo linachukua muda kidogo kutokana na mikopo hadi kukamilika kwake hupitia maeneo mengi.

Venelanda ambaye hata hivyo, hakutoa jibu la moja kwa moja kama mikopo kwa wanafunzi hao itaanza kutolewa lini, alisema HESLB itahakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa wanafunzi hao kabla ya kufunguliwa vyuo hivyo.

Mkuu wa Idara ya Habari Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, alipoulizwa na gazeti hili kama fedha za mikopo kwa wanafunzi wa  elimu ya juu zimeshapelekwa HESLB, alisema suala hilo waulizwe Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

“Bajeti ikishapitishwa bungeni, kinachobakia ni kwa wizara husika kushughulikia mipango yake, hivyo hata suala la fedha za mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu  wenye majibu ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,” alisema Mduma.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo, alipoulizwa na NIPASHE, alisema kimsingi mikopo bado haijaanza kutolewa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kufafanua kuwa kuanzia wiki hii wizara yake itaangalia uwezekano wa kushughulikia suala hilo ili wahusika wapewe mikopo hiyo.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Bhokombe Itembe, alisema wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanatarajia kuripoti chuoni hapo Oktoba Mosi, mwaka huu.

Alisema wiki iliyopita uongozi wa chuo na Daruso, walitaka kupanga vyumba katika hosteli kwa ajili ya wanafunzi, lakini zoezi hilo lilishindikana kwa sababu bado haijafahamika idadi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza watakaoripoti chuoni hapo.

Itembe alisema tatizo la kuchelewa kwa mikopo linatokana na sababu kadhaa, ikiwemo kutokuwepo kwa ushirikiano kati ya HESLB na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). “Mwanafunzi anapodahiliwa bila TCU kumuamulia ataenda chuo gani, huwezi kwenda na wakati huo huo bila HESLB kukupatia mkopo, vile vile huwezi kwenda chuoni,” alisema Itembe.

Rais wa Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha IFM, Michael Chazy, alisema chuo hicho kitafunguliwa Oktoba 8, mwaka huu na kwamba hadi sasa bado wanafunzi wanaoendelea na wale wa mwaka wa kwanza hawajaanza kupatiwa mikopo.

Naye Rais wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Paul Yunge, alisema suala la mikopo katika chuo lina utata hasa kwa wanafunzi wanaoanza mwaka wa kwanza ambapo baadhi yao wamejaza fomu vibaya na hivyo taasisi husika zinashughulikia tatizo hilo.

Rais wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Amos Chakushemeire, alisema utoaji wa mikopo hauridhishi kabisa katika chuo hicho ambapo wanafunzi walioanza muhula Julai, mwaka huu, wamelipwa robo ya mkopo wakati kiasi kingine cha mkopo hawajalipwa hadi sasa, hali ambayo imesababisha ukata mkubwa kwa wanafunzi.

“Chuo chetu ni tofauti na vingine, kina mihula mitatu, wanafunzi walioanza muhula wa Julai hawajalipwa sehemu nyingine,. Hivi karibuni uongozi wa chuo ulilazimika kuwakopesha Sh. 50,000 wanachuo hao ili kuwatuliza wasigome,” alisema Chakushemeire.

Rais wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Frank Nkinda, alisema mikopo ni changamoto kubwa katika chuo hicho ambapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawajapata mikopo hadi sasa. Alisema kutokana na hali hiyo, hivi karibu Mwenyekiti wa HESLB alifika chuoni hapo kuzungumza na uongozi, serikali ya wanafunzi na wanachuo ambapo alitoa ahadi kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika mwaka huu wa 2012/2013.

Mwaka jana serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitangaza utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo ambapo badala ya fedha hizo kutolewa kwa waombaji na HESLB, sasa fedha hizo zinapelekwa vyuoni ambako menejimenti za vyuo zinawajibika kuzisimamia na kuwapa waombaji. Hatua hiyo ilifikiwa ili kurahisisha mchakato wa kuwapatia fedha waombaji na pia kuepusha usumbufu kwa HESLB kutokana na wanafunzi kutoka vyuoni kuvamia ofisi hizo kwa lengo la kushinikiza wapewe fedha.

Taarifa iliyotolewa na HESLB na TCU Agosti 10 na 12, mwaka huu ilieleza kuwa zaidi ya wanafunzi 3,074 walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13, wameenguliwa katika maombi yao kutokana na dosari mbalimbali. Taarifa hiyo ilieleza kuwa HESLB pekee iliorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao ilibaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo.

Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo HESLB ilizibaini kwa walioenguliwa ni pamoja na kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa serikali za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.

Kwa upande wake TCU, iliwaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali. Miongoni mwa dosari ambazo zilitajwa na TCU ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano, miaka ya kumaliza masomo, mawasiliano sahihi kwa muombaji pamoja na uchaguzi wa masomo.

Hata hivyo, taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa. Kwa mwaka huu wa fedha 2012/13, serikali imeiongezea fedha HESLB kwa kuitengea Sh. bilioni 326 kwa wanafunzi 98,772.

Mwaka jana, serikali iliitengea HESLB Sh. 91,722,783,264  kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Ucheleweshaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu umekuwa ukisababisha wafanye migomo, vurugu na maandamano mara kwa mara kushinikiza walipwe.
Chanzo Nipashe

Monday, September 17, 2012

KUTOKA CBE DODOMA: MAJIBU YA WALE WOTE WANAOULIZIA RESULTS STATEMENTS


ESSAY COMPETITION FOR STUDENTS AND YOUNG PROFESSIONALS AGED 18-30



Essay Competition!!!!
Essay Guidelines
Who can participate:
Students and young professionals aged 18-30. Past CIPE Youth Essay Contest Winners are not eligible to participate.
Length and language 
 1,500-2,500 words. All essays must be in English.
Submission Format
All essays must be submitted through our online form and must include the writer's name in the file name and inside the document.
For example, if your name is John J. Smith, the document should be named "SMITH-JOHN.doc".
The essay you submit must focus on the role of youth and, where applicable, include examples from your personal experience relating to the topic. Essays that only talk about challenges to entrepreneurship in general terms, or limit proposed solutions only to what governments should do, will not be successful.
Winners: 
For each category, CIPE will publish the winning first, second, and third place essays. Winning authors will receive a $500 honorarium.
One grand prize winner will be invited on an all-expense-paid trip to attend CIPE's upcoming Democracy that Delivers for Entrepreneurs conference in the United States, which is planned for April 2013.
Deadline:
October 19, 2012 at 11:00 PM (EDT) 
Categories
The questions in bullet points are descriptive guidance meant to help you think about the topic. You do not necessarily have to answer these questions in your essay
Entrepreneurship and Innovation: Beyond technology
  • What barriers do young entrepreneurs in your country face in translating their ideas into products and services?
  • How do young entrepreneurs in your country foster new ways of acting and thinking?
  • What supporting institutions do young innovators need to succeed?
Inclusive Growth: The entrepreneurial environment for scaling up business
  • What challenges do youth-led businesses and entrepreneurs in your country face when they're expanding their enterprises?
  • What opportunities do youth-led businesses and entrepreneurs have to succeed in your country, and what are some of the success stories?
  • In your society, what tools or institutions do entrepreneurs need to grow small enterprises into larger, more prosperous businesses?
Social transformations: The role of entrepreneurs in building democratic societies
  • How can entrepreneurship among youth strengthen newly-formed or emerging democracies?
  • How are young entrepreneurs from different backgrounds participating in your country's democracy?
  • In what ways are young entrepreneurs contributing to social transformations in your country?
This message has been shared by GaryVero on behalf of Center for International Private Enterprises.

JOB OPPORTUNITIES FOR RECENT GRADUANTS: ACCESS BANK EXCITING CAREER OPPORTUNITIES IN MWANZA

AccessBank Tanzania is a full commercial bank providing micro, small and medium sized enterprises (MSMEs) with a broad range of appropriate financial services. Established in 2007, the bank is owned by a multinational shareholder group and member of an emerging global network of commercial microfinance banks (The "Access Group") with headquarters in Berlin/Germany.
 
As one of the fastest-growing bank in Tanzania, Accessbank is now opening soon a branch in Mwanza City, we offer excellent long-term career development opportunities for recent and fresh graduates and young professionals. In order to support our dynamic expansion process, we are looking forward to recruit a number of self-motivated and enthusiastic individuals to join our teams in our new branches in Mwanza.
 
FIELD OFFICERS
       Responsibilities:
  • Marketing and attracting potential business loan clients
  • Conducting on-site and risk assessment of loan applicants
  • Loan monitoring and recovery
Interested candidates must be ready to work extensively outside the office. If you prefer desk-based job, please look out for other vacancies advertised by the Bank from time to time.
 
       Qualifications and Experience:
  • Education: Graduate or Diploma holder
  • Experience: No prior work experience required
CLIENT ADVISOR
       Responsibilities:
  • Marketing and attracting potential clients for banking accounts and saving products
  • Opening closing, and maintaining different types of customers accounts
  • Dealing with cheques and money transfers
       Qualifications and Experince:
  • Education: Graduate or Diploma holder
  • Experince: No prior work experience required
CASHIERS:
       Responsibilities:
  • Cash deposit and withdrawal transactions (local and foraign currency)
  • Management and full responsibility of the daily cash box
       Qualifications and Experience:
  • Education: Diploma Holder or good form Six
  • Experince: No prior work experience required
Please send your CV ONLY by email to career@accessbank.co.tz DO NOT send CV more than once. Please refrain from sending any attachment via the website. Certificates and other relevant documents will only be required during the interview. The deadline for sending CVs is 1st October, 2012.

DO YOU WISH TO STUDY IN U.S? HERE ARE ANSWERS TO FREQUENTLY ASKED QUESTIONS....

How can I obtain a scholarship?: (Undergraduate)

 
Public Affairs Section of the American Embassy, Dar es Salaam offers no undergraduate scholarships. We have no funds available for study in the U.S., Tanzania or elsewhere.
American universities and private foundations may offer limited opportunities for exceptional candidates. The admission office of the university you wish to attend will be the best source of information on these opportunities.
 
Consult books in the library for information on financial aid for international students.
College Board International Student Handbook and Peterson's applying to Colleges and Universities in the United States, then visit the websites of the universities that interest you for further information.
 
When you write directly to a university or college for admission application materials, also request information on financial assistance. At some institutions your academic ability is considered together along with your financial need. At others your application for admissions and your financial need are considered separately.
 
Colleges and universities in the United States vary considerably in their admission standards and requirements. To be considered for admission in American universities, a student must be qualified to enter Tanzanian universities. To compete successfully for financial aid, students must have A' and B's on their A-level exams.
 
A student with 3 strong A levels, good O-level record and high SAT test results has the best chance of being offered a scholarship. In addition to the academics, a student who can demonstrate extracurricular interests (sport activities, clubs, hobbies, community projects) is also much appreciated. It will be up to the student to convince the admissions personnel of the institutions to which he/she is applying that he/she will be a real asset to that institution.
 
In order to make your applications competitive and convincing, use the guide books in our library, such as "Presenting Yourself Successfully to Colleges".
 
 For the student with exceptional ability in a particular sport, a sports scholarship could be an excellent way of financing his/her education. Write to the coach at a particular institution and correspond with him directly.
 
The student should be aware that acceptance by the coach or even the offer of a scholarship does not guarantee admission into the university/college. The regular admissions procedure must still be followed. The student should also be aware that he/she would still be expected to carry a minimum course load and maintain a certain academic average in addition to participating in the sports program.
 
Consult books in the library for in-depth information on how to apply for a sports scholarship.
 

How do I pay the college application and test registration fees?

For application fees and test fees, you should approach any bank's foreign exchange department so that an application can be made in order to obtain a US bank draft.
 
After gaining admission to an U.S. college/university, what college expenses will I incur?
There are several types of expenses which you will incur. The comprehensive cost of attendance per year ranges from about 12000 to 40000. A rough estimate is given below:
  • Tuition and fees this could range from $8,000 to $30,000.
  • Books and supplies $1,000 and above
  • Student's room & board (meals) $6,000 to $10,000
  • Personal (clothing, laundry, recreation, medical) $2,000
  • Transportation (If you do not live on campus.) $500
  •  

       To Be Continuing....

 

VIBE QUOTE OF THE DAY: BE ORIGINAL


Sunday, September 16, 2012

THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA: PRESENTS 20TH ANNIVERSARY 2012 ON 19TH SEPTEMBER.

EVENT THEME: "20 YEARS OF BRIDGING THE EDUCATIONAL GAP IN TANZANIA
AND BEYOND" 

MISS EXCELLENCE CHUO KIKUU HURIA TANZANIA 2012: HATIMAYE ZUENA NASEEB AVISHWA TAJI LA MISS EXCELLENCE OUT 2012

 
Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha kwa mlimbwende Zuwena Naseeb baada ya kuibika mshindi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Excellence wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) 2012, akiwabwaga wenzake tisa na kujinyakulia Kitita cha Shilingi 6,030,000 itakayomuwezesha kusoma Shahada ya Pili (Masters) katika Chuo Kikuu Huria Tanzania, shindano lililofanyika katika ukumbi wa Mwinyi uliopo kinondoni Biafra na kuhudhuriwa na watu na wadau mbalimbali wa maswala ya urembo.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa Naima Julius na nafasi ya tatu alinyakuliwa na mrembo Tela Alestas. Ambapo Mgeni rasmi katika shindano hilo la warembo wa OUT alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mh. William Lukuvi, ambae alimpongeza mrembo huyo kwa kuibuka mrembo lakini alimtaka kuchukua nafsi hiyo kukitangaza Chuo hicho na atumie nafasi aliyoipata ya kusoma Shahada ya pili vizuri ili kuja kuisaidia jamii yake na Taifa kwa ujumla.

Shindano hilo lililohudhuria pia na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Prof. Tolly Mbwete ambae alipata nafasi ya kuongea maneno machache, akianza kwa kumpongeza mshindi wa shindano hilo alimtaka atumie nafasi hiyo vizuri ikiwa pamoja na kukitangaza chuo. Makamu Mkuu huyo pia aliwapongeza waandaji na majaji wa shindano hilo kwa kufanikisha kufana kwake kwani hiyo imetokana na kazi yao nzuri.  

Katika pambano hilo la kila mwaka lililoshirikisha warembo kumi wa kutoka chuo hicho, upande wa burudani Banana Band chini ya Banana Ally Zoro alisimamia kuhakikisha wanaz ikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo. Kwa mwaka jana taji hilo la Miss Excellence OUT lilikwenda kwa Neema Mtitu ambae usiku wa jana alirithisha taji hilo kwa Miss Zuena Naseeb.


Tanzania Campus Vibe inapenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza Majaji kwa kazi kubwa na ngumu waliyoifanya na Pia kamati ya shidano hilo mwaka huu kwa kufanikisha kufana kwake. Pia tunapenda kuwapongeza warembo wote walioshiriki na kwa pekee Miss Excellence 2012, Zuena Naseeb. Mwisho kabisa pongezi zetu zinaenda kwa Uongozi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa juhudi zake za kuendeleza vipaji vya vijana chuoni hapo.

Mshindi wa Miss Excellence OUT 2012, Zuena Naseeb (aliyekaa) mara baada ya kuveshwa taji lake la umalkia wa shindano hilo mwaka huu, Kulia Ni mshindi wa pili Naima Julius na kushoto ni Mshindi wa tatu Tela Alestas
 
Miss Excellence OUT 2011, Neema Mtitu (gauni la njano) akimkabidhi shada la maua Miss Excellence OUT 2012 Zuena Naseeb hapo jana usiku mara ya baada ya kutangazwa mshindi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Mh. William Lukuvi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi 6,030,000 mshindi wa shindano la Miss Excellence OUT 2012, Zuena Naseeb, pesa ambayo itamuwezesha kusoma shahada ya pili (Master) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwete
   
Mgeni rsami Mh. William Lukuvi, Makamu Mkuu wa Chuo, Miss Excellence 2011 pamoja na warembo hao mshindi wa kwanza mpaka wa tano mara baada ya kukabidhi zawadi


Majaji wa shindano la Miss Excellence OUT 2012 wakifuatilia kwa makini shindano hilo usiku wa kumakia leo

Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora mara baada ya mchujo kufanyika
 
Burudani ya nguvu ilitolewa na warembo wote walioshiriki katika shindano hili, huu ulikuwa ni wimbo wa Bob Junior ujulikanao kama Nichum
 
Miss Excellence OUT 2012, Zuena Naseeb akiwa katika vazi lake la ufukweni
 
Mshindi wa pili wa shindano la Miss Excellence OUT 2012, Naima Julius ukionyesha vazi la ubunifu
 
Banana Ally Zoro akifanya makamuzi na bendi yake ya Banana Band