Leo tunaanza kukichambua Chuo Kikuu Cha kumbukumbu Cha Hubert Kairuki katika mfululizo wa makala zitakazokuwa zinakujia kila Ijumaa kuhusu Historia za Vyuo vikuu vyetu nchini Tanzania.
Prof. Hubert Kairuki Muasisi wa HKMU |
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha
Habert Kairuki (HKMU) ni moja kati ya vyuo vikuu vikubwa nchini Tanzania, ambacho
ndio chuo kikuu cha kwanza binafsi Tanzania kupata hadhi ya kuwa chuo kikuu, makao
yake makuu yapo jijini Dar es salaam, Chuo hiki kinachofundisha fani mbalimbali za maswala
ya Sayansi za Tiba tu kwa sasa.
Historia ya Chuo hiki ilianza
mwaka ya 1997 chini ya Mtandao wa Afya na Elimu (The Mission Mikocheni Health
AND Education Network (MMHEN)). Awali (HKMU) kilikuwa kikijulikana kama Chuo
Kikuu cha Kimataifa cha Mikocheni (Mikocheni Intenational University (MIU)). Muasisi
wa Chuo hiki ni hayati Prof. Hubert Kairuki ambae alikuwa ni Kaimu Mkuu wa Chuo
hicho, Prof. Hubert Kairuki alifariki mwaka 1999. Makamu mkuu wa pili
aliyechukua nafasi ya Prof. Kairuki alikuwa ni Prof. Esther Mwaikambo. Kwa sasa
Chuo hiki kipo chini ya Makamu Mkuu wa Chuo wake Prof. Keto Mshigeni ambae ni
mtaalamu maarufu duniani katika maswala ya kisayansi.
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya
Hubert Kairuki ndio chuo cha Kwanza binafsi Tanzania kupata hadhi ya kuwa Chuo
Kikuu kupitia Taasisi ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) mwezi Juni, 2000. HKMU pia
kinatambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), na pia kipo katika Muongozo wa Elimu
ya Tiba wa Kimatifa (IMED). Ambapo HKMU inajivunia kwa kuwa na Vifaa bora na
vya kisasa kwa ajili ya kufundishia na utafiti, maktaba yenye vitabu na yenye muongozo
wa kutumia kompyuta pamoja na huduma ya mtandao muda wote mwanafunzi awapo chuoni.
Mrs. Kokushubila Kairuki, Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini |
Kwa sasa HKMU kinatoa masomo
katika fani ya sayansi ya Afya tu, lakini mpango wa chuo ni kutanua wigo wa
elimu kwa kuanzisha masomo ya fani za sayansi na za kijamii. Kozi zinazofundishwa
kwa sasa ni Doctor of Medicine (MD), Shahada ya kwanza ya Uuguzi (BScN),
Diploma ya Uuguzi, na Cheti katika fani ya Wholistic Therapeutic Counseling
pamoja na kozi za awali zakuingia chuo kikuu (Pre-University Entry Programme).
HKMU pia kinatoa mafunzo katika
Postgraduate Diploma in Obstetrics and Gynecology, Postgraduate Diploma in Paediatrics
and Child Health, pamoja na Master of Medicine (M.Med). Pia kuna kozi katika
fani za Internal Medicine, Surgery, Obstetrics na Gynecology, Pediatrics na
Child Health.
HKMU kwa mara ya kwanza
kilifungua milango yake kwa umma mnamo tarehe 27 Agosti, 1997 kama chuo kidogo
lakini makini kilichojikita kutoa mafunzo kama chuo binafsi, dhamira yake ikiwa
ni kutoa wataalamu wa fani ya tiba za afya. Kwa muda huo sababu kubwa ya
kuanzishwa chuo hiki ni kupunguza upungufu wa wataalamu wa afya nchini Tanzania
kwa kufundisha madaktari na wauguzi katika ngazi ya cheti, diploma, shahada na stashahada.
Prof. Fredrick Kaijage,
Mwenyekiti
Baraza la Chuo
|
Tangu Tanzania inapata uhuru,
Afya, Umasikini na Ujinga ndio vitu vilivyokuwa maadaui wa Taifa hili, lakini
Serikali pamoja na asasi za kijamii pamoja na Taasisi za kimataifa hawakuweza
kufikia malengo katika kupambana na matatizo hayo makubwa ya Taifa hili. Watanzania wengi
walidharau majanga haya yanayoikumba Taifa lakini watu wachache hasa wasomi na
taasisi za kiafya zilizoanzishwa walichukua hatua za kimatendo kutatua Matatizo
hayo.
Moja ya wasomi alikuwa ni Hayati
Prof. Hubert C.M Kairuki ambae kabla ya HKMU kuanzishwa alikuwa ni mhadhiri
katika Kitivo cha Tiba, Chuo kikuu cha Dar es salaam. Nia yake ilionekana mwaka
1991 katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Tiba Tanzania (MAT) baada ya
kualikwa kama Mgeni Mkufunzi, alichukulia fursa hiyo kama sehemu ya kuelezea
mawazo yake juu ya matatizo yanayotukabili kama Taifa na pia kueleza hatua za
kuchukua kama wasomi katika kulinusuru Taifa juu ya matatizo hayo. Moja ni
kuelezea juu ya upungufu mkubwa wa
mafunzo ya Udaktari wa tiba Tanzania..
Prof. Keto Elitabu Mshigeni
Makamu Mkuu
HKMU
|
Kwa wakati huo akiwa kama
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mikocheni, Prof. Kairuki alipenda
kufanya vitu kwa matendo hivyo alianza maandalizi ya kuanzisha shule ya tiba
katika hospitali yake ya Mikocheni (MMH), Dar es salaam. Na mwaka 1992 katika sherehe
ya kuadhimisha miaka mitano ya Mission Mikocheni Hospital (MMH), Prof. Kairuki
alitangaza mipango ya ya Kuanzisha Chuo kikuu kitakachojulikana kama Chuo Kikuu
cha Kimataifa cha Siyansi ya Tiba cha Mikocheni (MIUHS).
Lakini baadae Prof. Kairuki
alitaka Chuo hiki kisiwe kinatoa masomo ya Siyansi ya Tiba pekee, hatua
iliyopelekea kubadilishwa jina kwa MIUHS na kusajiliwa kwa jina la Chuo Kikuu
cha Kimataifa cha Mikocheni (MIU). Baadae katika kuonyesha umuhimu wake na
kutoa heshima kwa muasisi wa Chuo hiki, uongozi wa chuo hiki uliamua kubadisha jina na Kukiita Hubert
Kairuki Memorial University (HKMU) Februari, 1999.
Prof. Paschalis G.N. Rugarabamu
Makamu Mkuu Msaidizi
Taaluma
HKMU
|
Tayari wanafunzi kutoka Tanzania,
Kenya, Uganda, Burundi, Zambia, Namibia, Uingereza na Nigeria wamesha hitimu
fani mbalimbali kutoka HKMU. Dhamira za Chuo hiki kwa siku za karibuni ni
kutanua uwigo wa fani kwa kuanzisha masomo ya fani mbalimbali kwa siku za hivi
karibuni ili kutimiza malengo ya Chuo hiki ya kuwa mfano wa kuigwa kwa vyuo
vingine Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kutoa elimu ya kiwango cha juu,
Tafiti za kina na kuwa mfano katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Chuo hiki kipo eneo la
Mikocheni jijini Dar es salaam kiwanja namba 322, Regent Estate, Barabara za
Ali Hassan Mwinyi na Old Bagamoyo, Kilometa 7 kutoka katikati ya jiji la Dar es
salaam. Ukiacha kuwa karibu kabisa na fukwe za bahari ya Hindi na Hoteli kubwa
za kitalii, chuo hiki pia kipo karibu kabisa na vivutio vingine vya kiutalii
nchini Tanzania.
Uongozi Pamoja na Wahadhiri wa HKMU katika moja ya Mahafali ya Chuo hiko. |
The
Hubert Kairuki Memorial University
P.O. Box 65300, Dar Es Salaam, Tanzania.
Physical Address:
Plot. No. 322 Regent Estate, Dar Es Salaam
6 th Floor MMHEN building
Tel.: +255-22-2700021 /4 ext 282 or 276 | Fax: +255-22-2775591
Email: info@hkmu.ac.tz ; v_c@hkmu.ac.tz ; secvc@hkmu.ac.tz
P.O. Box 65300, Dar Es Salaam, Tanzania.
Physical Address:
Plot. No. 322 Regent Estate, Dar Es Salaam
6 th Floor MMHEN building
Tel.: +255-22-2700021 /4 ext 282 or 276 | Fax: +255-22-2775591
Email: info@hkmu.ac.tz ; v_c@hkmu.ac.tz ; secvc@hkmu.ac.tz
No comments:
Post a Comment