Wednesday, September 19, 2012

KUTOKA HESLB: JUMLA YA WANAFUNZI 27,844 WAMEFANIKIWA KUPATA MKOPO KATIKA AWAMU YA KWANZA KWA MWAKA WA MASOMO 2012/13

Bodi ya ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) leo imetoa jumla ya majina 27,844 kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu juu hapa nchini kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kupitia tovuti yake www.heslb.go.tz.
 
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ilisema kwamba bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetoa awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mkopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013 ambao waliomba na kuwa na sifa za kupata mkopo.
 
Orodha hiyo ya majina inajumuisha Chuo ambacho mwanafunzi amesajiliwa na kiasi cha mkopo ambacho amepewa Mwanafunzi husika katika vipengele vyote vya mkopo kutokana na muongozo na vigezo vya kutoa mkopo kwa mwaka wa masomo 2012/2013.
 
WaomBaji wote wa Mkopo wanakumbushwa kwamba, pesa ya mkopo itatumwa katika Vyuo vyao husika ambapo watatakiwa kuweka saini zao ili kuthibitisha upokeaji wa mkopo. HAKUNA mwanafunzi atakae ruhusiwa kupokea mkopo bila ya kusaini pesa ambayo anatakiwa kupokea kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
 
Bonyeza  HAPA kuona majina hayo.
 


MUHIMU: TUMEAMUA KUKURAHISISHIA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZAKO AU ZA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKO. LIKE  Facebook PAGE YETU Tz CAMPUSVIBE Blog ALAFU TUTUMIE MAJINA YAKO YOTE MATATU NA CHUO ULICHOCHAGULIWA NA SISI TUTAFANYA KAZI YA KUKUTAFUTIA NA KUKUPATIA MAJIBU NDANI YA MUDA MFUPI. 
 

2 comments:

  1. mi natumia majina mawili tu....."WILLY CONSTANTINE...MZUMBE

    ReplyDelete
  2. S1074.0114.2009

    WILLY, COSTANTINE MU BACBAF 3,337,500

    ReplyDelete