Leo katika makala yako ya historia za vyuo vikuu tunakuletea historia fupi ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (The state University of Zanzibar) kwa kifupi kinajulikana kama SUZA. Chuo ambacho ikinapatikana katika mwambao wa Bahari ya Hindi katika mji mkongwe wa Stone Town huko visiwani Zanzibar.
SUZA kilianzishwa mwaka 1999 ambapo
mwaka mia miwili baadae yaani 2001 ndipo kilianza rasmi shughuli zake za
kitaaluma. Katika jitahada zake za kutoa elimu bora, SUZA kwa muda mfupi
kimeweza kufikisha lengo la kutoa elimu bora katika kanda ya nchi za Afrika.
Kama chuo kikuu cha umma, SUZA inalenga kutoa elimu husika kwa walengwa katika
kuharakisha mabadiliko ya kijamii na mabadiliko chanya ya kuchangia maendeleo
ya kiuchumi na kisiasa.
Dr. Ali Mohammed Shein Mkuu wa Chuo (SUZA) |
Chuo hiki kimeanzishwa chini ya
kifungu Na. 18 sheria ya mwaka 1999 ya baraza la wawakilishi Zanzibar. SUZA
kimenzishwa ili kuendesha kozi zitakazo zalisha walimu wenye utaalamu ambao
watafundisha katika shule za sekondari pamoja na kulinda, kuwezesha, na
kusambaza elimu katika masomo ya sanaa, sayansi na teknolojia.
Ikiwa ni miaka kumi sasa toka
kuanzishwa kwake, SUZA kimejitanua zaidi kwani kina matawi mawili na kipo
mbioni kufungua tawi la tatu yote yakiwa katika visiwa vya unguja. Tawi kongwe
kabisa ni lile la Beit-el-Rasi, tawi liliotakana na chuo cha kwanza cha uwalimu
Afrika Mashariki. Tawi hili lipo pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi, umbali
wa kilomita tano kutoka mji mkongwe wa Stone Town.
Tawi lengine ni tawi la Vuga, lilipo
kati kati ya mji wa Stone Town, ni majengo ya kihistoria yanayotumiwa na Chuo
hiki katika tawi la Vuga na kukifanya kivutie kwa mazingira yake. Tawi la Vuga
limezungukwa na na huduma za kijamii pamoja na ofisi za umma.
Dr. Ahmad Hamada Khatibu Makamu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Utwala na Fedha (SUZA) |
Prof. Idris A. Rai Makamu Mkuu wa Chuo (SUZA) |
Hivi karibuni SUZA inatarajia kuongeza
Tawi lengine katika shabaha ya kuongeza wigo wa kutoa elimu bora, Tawi la
Tunguu ni tawi la tatu na jipya litakalofunguliwa hivi karibuni. Tawi hili lipo
umbali wa Kilomita 12 kutoka mji wa Stone Town. Mandhari yake ya kijani, tawi
hili linalifanya liwe na miundombinu bora na ya kuvutia yenye kiwango cha
kimataifa. Mipango ya chuo ni kuongeza matawi mengi zaidi ndani ya kipindi cha
miaka mitano ijayo.
SUZA ni moja kati ya chuo
kinachoongoza katika Visiwa vya Zanzibar, hii inatokana na ukuaji wa haraka wa
chuo hiki ambapo kila mwaka kuna ongwezeko la wanafunzi wanaojiunga na chuo
hiki. Kwa chuo kidogo kilichoimarika hivi karibuni, sasa chuo kina wanafunzi
1,205 na kati ya hao wanafunzi 693 wanasoma shahada ya kwanza katika fani
mbalimbali.
Mrs. Ramla Mohammed Mlezi wa wanafunzi |
Kwa sasa Chuo kina Taasisi ya
Kiswahili na Lugha za kigeni ambapo raia kutoka ndani na nje ya nchi wanapata
kujifunza lugha mbalimbali duniani, Shule ya Uwalimu, Sanaa na Sayansi (SEAS),
Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza (Institute of Continuing Education), na Chuo
cha Kompyuta. Chuo kinatarajia kufungua shule mbalimbali huko baadae katika
njia ya kujpanua zaidi.
Majengo mapya ya SUZA yanaomaliziwa kujengwa ya katika Tawi la Tunguu, visiwani Unguja |
No comments:
Post a Comment