Friday, September 14, 2012

KUTOKA SUZA: IKIELEKEA KUSHEHEREKEA MIAKA 10 TOKA KUANZISHWA KWAKE, SUZA (THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR) CHAPOKEA TUZO YA UKUAJI WA KITAALUMA TOKA CISCO NETWORKING

Kikiwa kinaelekea kuadhimsha miaka 10 toka kuanzishwa kwake Chuo kikuu cha Zanzibar, SUZA (The State University of Zanzibar) kimetunukiwa tuzo ya ukuaji wa kitaaluma na shirika la CISCO Networking baada ya shirika hilo la Kimataifa la kitaaluma kuona juhudi za Chuo hiko katika kutoa elimu bora tangu kuanzihswa kwake.

SUZA ambacho  kilinza miaka kumi iliyopita kimetangaza kupitia mtandao wake kwamba mwaka huu chuo hicho kitasheherekea miaka kumi tangu kuanzishwa kwake kuanzia mwezi Septemba kilele cha sherehe hizo kitakuwa ni siku ya Mahafali ya saba ya chuo hicho Disemba 24, 2012. Sherehe hizo zinaendana na mipango mipya ya  kuongeza college mpya pamoja na kuongeza kozi mpya za masomo chuoni hapo na kuendelea kutimiza kauli mbiu yake ya "Ni muda wa Kukua".

SUZA ni moja kati ya Vyuo vikubwa na vinavyoendelea kwa kasi katika visiwa vya Zanzibar chenye maskani yake katika mji wa kihistoria wa Stoine Town. Chuo hiki kwa sasa kina wanafunzi 1,205 ambapo 693 ni wanafunzi wa shahada ya kwanza.

Tanzania Campus Vibe Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza SUZA kwa mafanikio waliyofikia na mchango wao wa kutoa elumu bora hapa nchini.
 

No comments:

Post a Comment