Tangu mwaka 2005 kumekuwepo na
tatizo la kutofautiana kwa Mihula ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mpaka cha
Nne, Kidato cha Tano na Sita na Vyuo vya Ualimu. Aidha, kipindi cha kufanya
mitihani ya Taifa katika kidato cha Nne na Sita hutofautina. Vilevile,
usahihishaji wa mitihani ya ngazi hizo za elimu umekuwa ukifanyika wakati
baadhi ya makundi ya wanafunzi wakiendelea na masomo Shuleni/Vyuoni.
Usahihishaji wa mitihani wakati
baadhi ya makundi ya wanafunzi wakiendelea na masomo umekuwa ukiathiri
maendeleo ya wanafunzi kimasomo. Wasahihishaji wa mitihani hiyo wamekuwa na
muda mrefu wa kufanya kazi hiyo na kukosa muda wa kupumzika na kujikuta wanafanya
kazi hiyo kwa mfululizo mwaka mzima. Hali hiyo imesababisha baadhi ya walimu
kushindwa kufanya kazi za kitaaluma ipasavyo.
Ili kurekebisha hali hiyo
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeamua kurekebisha Mihula ya shule; ili
wanafunzi wa ngazi zote katika shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu
wawe na vipindi vya likizo vinavyofanana.
Aidha, urekebishaji wa Mihula
utaendana sambamba na marekebisho ya vipindi vya mitihani ya Taifa katika ngazi
hizo kama ifuatavyo:
Tanbihi: Wanafunzi wote watapumzika
Mwezi Juni na Desemba. Waraka huu, unaanza kutumika tarehe 01 Januari, 2013 na
kufuta Waraka wa Elimu Na. 5 wa Mwaka 2004
M. M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
Katibu Mkuu,
OWM -TAMISEMI,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
Mkurugenzi,
Taasisi ya Elimu ya Watu
Wazima,
S.L.P. 20679,
DAR ES SALAAM.
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Elimu Tanzania
S.L.P. 35094,
DAR ES SALAAM.
Katibu Mtendaji,
Baraza la Mitihani la Tanzania,
S.L.P. 2624,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment